+255 716 503 084
info@liwopac.or.tz
P.O.Box 408 Lindi, Tanzania
Home
ABOUT
About Us
Project
Our Project
LIWOPAC- Goal
LIWOPAC- Gallery
EVENTS
Upcoming Events
Report & News
Report & News
Contact
Donate Now
Gallery
Mnufaika wa mradi wa Child Care Support Bahati Mtocha wa Nachingwea ambaye ni mwanafunzi wa kozi umeme katika chuo cha Masasi FDC akipokea chakula lishe kutoka shirika la LIWOPAC
Mratibu wa mradi wa kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa wanawake & vijana unaofadhiliwa na shirika la OXFAM GB Bw. Mwendo Mnambala akitolea ufafanuzi wa namna mradi unavyofanya kazi katika ziara ya mafunzo ya shirika la PINGOs Forum iliyofanyika 07.07.2021 jijini Arusha
Afisa mradi wa shirika la LIWOPAC Dada. Fatuma Nyama akieleza namna shughuli za msaada wa kisheria zinavyofanyika katika mkoa wa Lindi kupitia shirika la LIWOPAC. Ameyaongea haya katika ziara ya mafunzo iliyofanyika jijini Arusha katika shirika la PINGOs Forum
Bw. Mwendo Mnambala kwa niaba ya mkurugenzi wa LIWOPAC akikabidhi baiskeli ya kutembelea walemavu kwa dada Huzwaima Saidi (13) mkazi wa Kijiji cha Kilolambwani, kata ya Kilolambwani ndani ya manispaa ya Lindi ambaye ni mwanafunzi wa darasa la 5 katika shule ya msingi Kilolambwani.
Wanafunzi wa kike wa chuo cha maendeleo Masasi (Masasi FDC) baada ya kukabidhiwa taulo za kike (SODO) kwa ajili ya matumzi yao pindi wawapo chuoni.
Pichani ya maskani ya vijana katika mtaa wa Mpilipili manispaa ya Lindi katika kujadili mila potofu zinazo mkandamiza mwanamke ndani ya mkoa wa Lindi. Shughuli iliratibiwa na redio mashujaa FM kwa ushirikiano mkubwa na shirika la LIWOPAC
Msaidizi wa kisheria Dada Somoe Mpochi akitoa msaada wa kisheria kwa mteja Mzee Mchonyo ambaye alifika ofisini LIWOPAC kutoa malalamiko ya matunzo ya watoto kwa mzazi mwenza
Mratibu wa mradi wa CHILD CARE SUPPORT Bw. Jonaphrey Pembe akiwakabidhi bima ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mingoyo kutokana na jitihada zinazofanywa na LIWOPAC kusaidia watoto kielimu mkoani Lindi
Washiriki wa ziara ya mafunzo jijini Arusha kwa shirika la PINGOs Forum wakitabasamu baada ya majadiliano ya kufurahisha. Hii ni siku ya mafunzo ambayo yalifanyika eneo ya Mtoa wa MBU lililopo wilayani Monduli – Arusha.